Tuesday, September 28, 2021
   
Text Size

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema njama zinazofanywa na watu wasio waaminifu kwenye michakato ya ununuzi wa umma ni kikwazo katika kupata thamani ya fedha kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akifungua Kongamano la Nane la Mwaka la Usimamizi katika Ununuzi wa Umma, lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA). Kongamano hilo la siku mbili (kuanzia tarehe 26 – 27 Mei, 2021) lililokuwa na Kauli Mbiu ‘Maboresho ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma Nchini Tanzania: Mafanikio na Changamoto zake’ lilihudhuriwa na Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi za Taasisi Nunuzi, Maafisa Masuuli, Mameya na Wenyeviti wa Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri pamoja na Madiwani.

Dkt. Nchemba amesema kuna njama zinazofanywa kwa umakini mkubwa na watu hao, huku wakihakikisha wanazingatia sheria na taratibu ili wasibainike. “Kuna njama kwenye michakato ya ununuzi wa umma zinafanywa kwa kiwango cha juu, na ukifuatilia unakuta watu wamezingatia sheria na taratibu, lakini ndani yake kunakuwa na njama,” alisema Dkt. Nchemba.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Balozi Dkt. Matern Lumbanga alitoa rai kwa wadau wote wa ununuzi wa umma kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kuzingatia sheria, kwa kuwa hilo sio suala la hiari, huku akiahidi kuwa PPRA itaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali kuhakikisha inatekeleza kikamilifu majukumu yake ya kusimamia sheria ya ununuzi wa umma.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo, alisema Mamlaka hiyo imeisaidia Serikali kuokoa takribani shilingi bilioni 30 ambazo zingepotea kutokana na kutofuatwa kwa taratibu za ununuzi na hasa katika eneo la usimamizi wa mikataba, katika Mwaka wa Fedha 2017/18 hadi 2019/20.

“Sehemu ya fedha zilizookolewa zinatokana na malipo wakandarasi na watoa huduma kinyume na utaratibu na hivyo taasisi hizo kuelekezwa kurejesha fedha hizo,” alisema Mhandisi Kapongo.

En cilgin hd porno videolari icin sitemizi ziyaret ediniz.Yerli yabanci escort bodrum kizlari burada