Thursday, December 02, 2021
   
Text Size

Matumizi ya mfumo wa ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao (Taneps) yameiwezesha Serikali kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 60 kati ya fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera, alipokuwa akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi cheti mshindi wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, iliyofanyika katika makao makuu ya tume hiyo jijini Dodoma.

Dkt. Mahera alisema mchakato wa ununuzi wa vifaa vya uchaguzi huo, uliohusisha wazabuni kutoka ndani na nje ya nchi, ulifanyika kwa uwazi na ushindani mkubwa kutumia mfumo wa taifa Taneps, unaosimamiwa na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA).

“Matumizi ya mfumo huo yamesaidia katika kupungua kwa bajeti ya ununuzi wa vifaa vya uchaguzi kutoka shilingi bilioni 331 hadi shilingi bilioni 268,” alisema Dkt. Mahera na kuongeza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 uliendeshwa kwa kutumia fedha za ndani peke yake.

En cilgin hd porno videolari icin sitemizi ziyaret ediniz.Yerli yabanci escort bodrum kizlari burada