Wednesday, March 03, 2021
   
Text Size

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Bunge, Bw. Tixon Nzunda, amewataka viongozi wa taasisi za Serikali kutonyamazia vitendo vya rushwa na ubadhirifu kwenye ununuzi wa umma

Bw. Nzunda aliyasema hayo alipokuwa akizindua Mwongozo wa Kuzuia Rushwa katika Ununuzi wa Umma jijini Dodoma. Alieleza kuwa baadhi ya viongozi hao wamekuwa na tabia ya kukaa kimya dhidi ya vitendo vya rushwa ambavyo utafiti umeonesha kuwa vimekuwa vikitokea kwa kiwango kikubwa katika michakato ya ununuzi.

Alifafanua kuwa utafiti huo, uliofanywa wakati wa kuandaa mwongozo huo, umebaini kuwa maeneo yenye kiwango kikubwa cha viashiria vya rushwa ni pamoja na uandaaji wa zabuni, uandaaji wa orodha ya wazabuni, mfumo wa tathmini, maandalizi ya bajeti za zabuni na usimamizi wa mikataba

“Katika eneo hili la ununuzi wa umma, wakati mwingine halizungumzwi sana. Nilikuwa nateta na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), anasema eneo hili likifika hapa wakubwa wengi hawataki kuzungumza sana juu ya rushwa. Na wakubwa wengi hawataki kuzungumza sana juu ya maadili, wakubwa wengi hawataki kuzungumza sana juu ya mgongano wa maslahi. Hapo tuna-mute (tunanyamaza),” alisema Katibu Mkuu.

“It is a high time (umefika muda sasa) tuunge mkono juhudi za Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali kwa ujumla, kuanza kuwa na mjadala wa wazi kuhusu rushwa katika ununuzi wa umma,” aliongeza Bw. Nzunda.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema kuwa muongozo huo ni matokeo ya utashi na dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye wakati wote amekuwa mstari wa mbele katika kuongoza mapambano dhidi ya rushwa nchini.

“Dhamira hii inadhihirishwa pia na uwepo wa mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa ukiwemo mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu wa Mwaka 2017-2022, ambapo TAKUKURU ni miongoni mwa watekelezaji wa mkakati huu,” alisema Brig. Jen. Mbungo.

“Mwongozo huu una lengo la kuziba mianya ya rushwa kwenye manunuzi na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu ili kuhakikisha ubora na thamani ya manunuzi husika. Aidha, mwongozo huu unatarajiwa kutumika kama daraja kati ya wadau na Takukuru ili kuimarisha ushirikiano, umoja na ushirikiano katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa katika ununuzi wa umma,” aliongeza Mkuu huyo wa Takukuru.

Naye Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Ukidhi wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Ayub Kasuwi, aliyemuwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo kwenye uzinduzi huo, alisema ushirikiano kati ya taasisi hiyo na Takukuru umezaa matunda katika kuongeza ukidhi wa sheria ya ununuzi wa umma.

“Pamoja na ukweli kwamba bado kuna changamoto ya rushwa katika ununuzi wa umma, lakini ushirikiano uliopo kati ya PPRA na Takukuru umechangia kwa kiasi kikubwa kudhibiti mianya ya rushwa kwenye ununuzi wa umma, kwani kiwango cha ukidhi wa sheria ya ununuzi wa umma kimeongezeka kutoka asilimia 39 katika Mwaka wa Fedha 2006/2007 na kufikia asilimia 78.8 katika Mwaka wa Fedha 2019/2020,” alisema Mhandisi Kasuwi.

Aliongeza kuwa PPRA inaamini kuwa kadiri ukidhi wa sheria ya ununuzi wa umma unavyoongezeka ndivyo mianya ya rushwa inavyozidi kupungua.

Mwongozo huo uliozinduliwa Novemba 24, 2020 utasambazwa kwa taasisi nunuzi zote pamoja na wadau wa sekta hiyo.

En cilgin hd porno videolari icin sitemizi ziyaret ediniz.Yerli yabanci escort bodrum kizlari burada